TUPSE
TUPSE ni chama cha wafanyakazi sekta ya ulinzi binafsi hapa nchini
Dhumuni letu
Ni kujenga nguvu ya pamoja katika kutetea, kulinda na kusimamia haki ma maslahi ya chama.
Imani Yetu
Wafanyakazi Duniani kote ni sawa na wana haki ya kushirikiana na wenzao katika kulinda umoja wao na kudai haki na maslahi yao.

Chama cha Walinzi Binafsi Tanzania (TUPSE) ni chama kinachoundwa na Wafanyakazi wote wa Sekta ya Ulinzi Binafsi Tanzania. Hivyo Basi wafanyakazi wote sekta ya ulinzi binafsi hapa nchini mnapewa wito kujiunga na TUPSE ili kuboresha hali za kazi, kupata msaada wa kisheria, lakini pia kukuza na kuinua maslahi ya pamoja ya wafanyakazi katika sekta hii.

DHUMUNI KUU LA TUPSE

Kujenga nguvu ya pamoja katika kutetea, kulinda na kusimamia haki ma maslahi ya chama.

Kuwa chama imara, chenye nguvu, cha kidemokrasia, kinachojitegemea, kinachounganisha wafanyakazi wote kutoka sekta za ulinzi zinazowakilishwa ndani ya TUPSE, kinachotimiza haki na matazamio ya wanachama wake kwa kukidhi mahitaji yao ya kijamii.

Kuwa chama kinachotimiza haki na matazamio ya wanachama wake kwa kukidhi mahitaji yao ya kiuchumi na kijamii.

0

Miaka ya Uzoefu

1000+

Idadi ya wanachama

Chama cha wafanyakazi walinzi

Malengo ya Chama cha Wafanyakazi TUPSE

Haki

Kulinda na kutetea haki na maslahi ya Wanachama.

Hali nzuri za Kazi

Kuboresha na kuendeleza hali nzuri ya Wanachama katika maisha yao wakiwa kazini.

Kutatua Migogoro

Kujadiliana na Mwajiri kwa lengo la kuondoa tofauti zinazojitokeza baina ya Waajiri na Waajiriwa na kati ya Mwajiriwa mmoja na mwenzake.

Utoaji Elimu

Kutoa elimu juu ya masuala mbali mbali ya kikazi, ikiwa ni sambamba na kuwaelimisha wanachama juu ya haki/wajibu wao wawapo kazini, kupitia semina, matamasha, na mikutano.

Ufingaji Mikataba ya hali Bora za kazi

katika uboreshaji masilahi ya wafanyakazi chama kitajikita katika kujadiliana na waajiri, serikali kwa lengo la kuhakikisha masilahi bora kwa wanachama yanapatikana, ili kuendana na gharama za maisha.

Msaada wa Kisehria

Kutoa msaada wa kisheria/ uwakilishi pale mwanachama anapopatwa na changamoto katika kazi yake, ikiwa ni sambamba na kuachishwa kazi pasipo sababu/taratibu kufuatwa.

Ushirikiano

Kushirikiana na Vyama vingine vya wafanyakazi nchini na kuhakikisha kuwa kwa ushirikiano huo haki za wafanyakazi zinalindwa kutetewa kwa pamoja. Na Kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha na kuimarisha ulinzi wa watu na mali zao.

TAASISI ZA SERIKALI TUNAZOSHIRIKIANA NAZO

Kwa kutambua kwamba Wafanyakazi Sekta ya Ulinzi Binafsi Tanzania katika utendaji wa shughuli zao wamekuwa wakisimamiwa na mamlaka mbili ambazo ni; Wizara ya Mambo ya Ndani ambayo kwa kiasi kikubwa inasimamia mifumo ya kiutendaji pamoja na vifaa vya kazi kama vile Siraha za Moto n.k. katika Makampuni haya; na Ofisi ya waziri mkuu(Kazi,Vijana,wazee, ajira, watu wenye ulemavu) ambayo kwa kiasi kikubwa imejikita katika kusimamia Sera, Sheria, Kanuni na Miongozo mbali mbali kuhusiiana na masuala ya kiajira.

SHABAHA YETU

Kuwa chama bora kwa wafanyakazi wetu

Shabaha kuu ya chama ni kushirikisha wanachama katika maamuzi, kushinikiza kuwepo kwa sera za kuongeza na kupanua wigo wa nafasi za ajira, kuboresha mazingira ya kazi na kuhakikisha kuwa wanachama wanamudu maisha yao wakiwa ndani ya ajira na wakistaafu.

Jisajili Uwe mwanachama wetu!!

Bonyeza kitufe hiki kuweza kupakua fomu ya kujiunga ambapo ada ya uanachama ni 2% ya mshahara halisi wa mfanyakazi. Ada hii utaichangangia kila mwezi

Tuandikie maoni yako! Nasi tutayafanyia kazi...

Wasiliana Nasi

Tupo JENGO LA MACHINGA COMPLEX Ghorofa ya 3, chumba namba 32

Anuani Yetu

S.L.P. 25175 Dar es salaam Office Makao Makuu

Tel. +255 743 183 708 kanda ya Dar es salaam

Tel. 0 736 202 481 +255 736 202 481 0743 183 708 0653073341

Masaa ya kazi

TUPSE@2023

Scroll to Top